December 15, 2013





Simba imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya KMKM ya Zanzibar.

 
Katika mchezo huo uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, Simba ilionyesha kubadilika.
Mabadiliko makubwa ya Simba yalikuwa ni uchezaji wa kasi na kupeleka mashambulizi mengi.

Mabao ya Simba katika mechi hiyo yalifungwa na Christopher Edward, Said Ndemla na mkongwe Henr Joseph akafunga la tatu kwa mkwaju wa penalti.

Simba imecheza mechi yake ya kwanza ikiwa chini ya Kocha mpya, Zdravko Logarusic raia wa Croatia.

Jana, KMKM iliwapa wakati mgumu mabingwa wa Tanzania ingawa mwisho walipoteza kwa kufungwa mabao 3-2.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic