Kocha Mkuu wa Simba, Zravko Logarusic
amesema hana nia mbaya na wachezaji atakaowaacha.
Badala yake anataka kuimarisha kikosi
chake kwa ajili ya mechi 13 zilizobaki za ligi na nyingi za mashindano.
“Tuna muda mchache sana na tunahitaji
wachezaji wa aina fulani, hivyo sina ugomvi wala matatizo na nitakaowaacha.
“Wanatakiwa kuelewa tunafanya nini na
ukichaguliwa maana yake umeonyesha uwezo,” alisema.
Kocha huyo ameamua kupunguza kikosi
chake na kubakiza wachezaji wachache watakaowania namba kwa ushindani na
kuisaidia Simba kurudisha hadhi yake.
Logarusic raia wa Croatia amechukua
nafasi ya Abdallah Kibadeni ambaye sasa ametua Ashanti United.







Inawezekana akatusaidia kwa kiasi fulani
ReplyDelete