| SIKU AZAM TV ILIPOSAINI MKATABA NA TFF NA BODI YA LIGI KUPATA HAKI ZA KUONYESHA LIGI KUU TANZANIA BARA. |
Azam
Media Ltd leo imepata leseni kutoka Mamlaka ya
Mawasilino Tanzania (TCRA) na hivyo kuwa na uwezo wa kuanza rasmi shughuli zake
hapa Tanzania.
Hatua hii
muhimu sasa inaiwezesha AzamTV kuanza kutoa huduma zake kwa wateja wake kote
Tanzania kuanzia tarehe16 Desemba.
Huduma hii itwapa fursa wateja kuangalia
zaidi ya chaneli 50 za kitaifa na kimataifa ziliozosheheni burudani kwa ajili
ya familia kwa bei nafuu ya shilingi 12,500/= kwa mwezi. Kutakuwepo wigo mpana
wa kuchagua kifaacho kuangalia vikiwemo vipindi vya michezo, makala, watoto na
tamthilia kutoka Tanzania, barani Afrika na sehemu mbalimbali za
dunia. Baadhi ya vipindi hivyo tajwa vitapatikana katika chaneli
maarufu kama vile National
Geographic Gold na Nickelodeon, na pia
matangazo yetu yatakuwa na chaneli za bila malipo zikiwemo TBC1, Channel 10,
Clouds, ZBC na K24.
Jambo la
kusisimu zaidi ni kwamba AzamTV
itakuwa na matangazo katika chaneli zake tatu:
AzamOne -
Itakuwa na vipindi vya kiafrika, ambapo kwa asilimia kubwa vitahusu masuala ya
Afrika Mashariki kwa lugha ya Kiswahili. Hii ndiyo chaneli ambayo itakuwa
ikirusha matangazo ya Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara;
AzamTwo –
Hapa vitapatikana vipindi vya burudani kwa familia amabavyo ni vya kimataifa na
baadahi ya hiovyo vitakuwa katika lugha ya kiswahili;
SinemaZetu –
Chaneli maalum kwa ajili ya tamthilia za kitanzania.
Mtendaji Mkuu
wa Azam Media, Rhys Torrington, alisema: “Huu ni wakati wa kujivunia kwa Tanzania kwani sasa ina huduma za luninga
zinazopatikana kwa bei ambayo wengi wanaweza kuimudu. Miezi michache ijayo tutaivusha huduma hii
mipaka hadi katika nchi zingine za Afrika Mashariki na hata mbali zaidi.
Nimefarijika kwamba tumewekeza vilivyo katika chombo hiki cha kitanzania na
tutaendelea kufanya hivyo”.
Torrington pia alibainisha kuwa kwa wateja ambao
hawatapenda kungojea kuzinduliwa rasimi wa huduma za Azam TV, milango ya ofisi
zake za Dar es Salaam itakuwa wazi kuanzia leo (Ijumaa
Desemba 6, 2013). Wateja wataweza
kununua vifaa muhimu kutoka duka la AzamTV na kwa
mawakala walioidhinishwa na hivyuo kuweza kujionea vipindi mbalimbali
kuanznia sasa – japo malipo yao kwa mwezi yatahesabiwa kuanzia Desember 16.







I really loved reading your blog. It was very well authored and easy to understand. Unlike other blogs I have read which are really not that good.Thanks alot!
ReplyDeletegogoro s2