Kamati ya Sheria na Hadhi za
Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imekutana Jumamosi
(Desemba 28, 2013) kujadili mambo mbalimbali yaliyofikishwa mbele yake ikiwemo
usajili wa dirisha dogo ambapo klabu zenye matatizo zimepewa hadi Januari 10
mwakani kurekebisha.
Baadhi
ya klabu ikiwemo Simba zimezidisha idadi ya wachezaji, hivyo zimepewa hadi muda
huo kupunguza ambapo zikishindwa kazi hiyo itafanywa na Kamati yenyewe.
Simba
ina nafasi tano za kujaza kwenye dirisha dogo lakini imewasilisha majina ya
wachezaji sita.
Pia
klabu nyingine zimetakiwa ama kuvunja mikataba ya wachezaji au kuendelea kuwa
nao, na si kuendelea kuwalipa mishahara wakati imeshawaondoa katika orodha yao.







0 COMMENTS:
Post a Comment