Wanachama
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wametakiwa kuheshimu uamuzi
halali unaofanywa na vyombo vyake kwa kuzingatia katiba na kanuni zake.
Kamati
ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF imetoa maelekezo hayo baada ya klabu ya
Stand United kukata rufani kupinga uamuzi wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB)
kuagiza mechi yao ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) dhidi ya Kanembwa JKT
iliyovunjika kurudiwa Februari Mosi mwakani mjini Tabora.
Sekretarieti
ya TFF iliwasilisha suala hilo kwa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ili
itoe mwongozo kwa vile uamuzi huo uliofanywa na TPLB hauwezi kukatiwa rufani
kwa mujibu wa Kanuni za ligi husika.
Kamati
imesisitiza kuwa hiyo ni falsafa ya mpira wa miguu ambapo uamuzi unaofanywa
uwanjani haukatiwi rufani, hivyo uheshimiwe kama ilivyo kwa masuala ya mpira wa
miguu kutopelekwa katika mahakama za kawaida za kisheria.

0 COMMENTS:
Post a Comment