Klabu ya
Yanga imeingia mkataba na Kampuni ya MGB Agency ya Zamalek, Cairo ya kuuza
mechi yao ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya El Ahly ya nchini Misri ikiwa
watasonga mbele katika hatua ya awali ya michuano hiyo.
Mechi hiyo ya
mzunguko wa pili wa michuano hiyo, kama Yanga itafanikiwa kuwaondoa wapinzani
wao Komorozine ya Comoro, itachezwa Januari 16, mwakani kwenye Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu
wa Yanga, Beno Njovu, amesema mechi hiyo wameiuza kwa dola 55,000 (Sh milioni
88).
Njovu alisema
mkataba huo walioingia nao ni kwa mechi moja pekee itakayochezwa Dar es Salaam.
“Tumeiuza
mechi yetu ya mzunguko wa pili mara tutakapovuka na kukutana na wapinzani wetu
El Ahly, tumeiuza kwenye Kampuni ya MGB ya nchini huko. Hivi sasa tupo kwenye
mazungumzo na televisheni tutakayoipa tenda ya kurekodi mechi hiyo na kuirusha
moja kwa moja Misri,” alisema Njovu.
Kwa upande wa
mwakilishi wa kampuni hiyo, Francis Gaitho, alisema kuwa tofauti na Misri nchi
nyingine zitakazotazama mechi hiyo ni zilizopo Ukanda wa Afrika Magharibi na
Afrika ya Kati.
0 COMMENTS:
Post a Comment