Kikosi cha UITM FC anachokichezea Abdi Kassim ‘Babi’ kimeanza
vibaya michuano ya Kombe la FA nchini Malaysia baada ya kulala kwa mabao 3-2.
Mechi hiyo iliyochezwa jana, UITM FC
ililala kwa mabao hayo huku Babi akiwa kati ya wachezaji wa kikosi cha kwanza.
Akizungumza mara tu baada ya mchezo huo,
Babi aliyewahi kukipiga Mtibwa Sugar, Yanga na Azam FC alisema mechi ilikuwa
ngumu.
“Nimefanikiwa kutoa pasi za mabao yote
mawili, lakini jamaa walinibana ile mbaya. Pale katikati wana Wabrazil wanne,
kwa hiyo haikuwa kazi lahisi,” alisema Babi.
0 COMMENTS:
Post a Comment