Katika kuhakikisha wachezaji wa Simba
wanaelewa kile kinachofundishwa, kocha mkuu wa timu hiyo, Zdravko Logarusic,
amekuwa akitumia neno moja la Kiswahili.
Kocha huyo ambaye ni raia wa Croatia, ameonyesha
kuwa ni mwepesi wa kujifunza, kitu ambacho kimekuwa kikiwasumbua makocha
wengine.
Katika mazoezi ya juzi yaliyokuwa
yakifanyika kwenye Uwanja wa Kinesi jijini Dar, Loga alikuwa akikorofishana na
wachezaji wake mara kwa mara kutokana na wengi wao kuonyesha kuwa hawamuelewi.
Kila mara kocha huyo ambaye amewahi
kuifundisha timu ya Gor Mahia ya Kenya, alikuwa akitumia neno ‘piga’ pale
alipokuwa akimtaka mshambuliaji au beki kupiga mpira.
Hata hivyo, mara kwa mara alikuwa
akimuita kiungo wa timu hiyo, Amri Kiemba, ili awe mkalimani wake na kumtumia
kuwaelewesha baadhi ya wachezaji kwa Kiswahili pale alipoona kuwa hawamuelewi.
0 COMMENTS:
Post a Comment