Kocha wa Ashanti, Abdallah Kibadeni,
ameponda kiwango hafifu kilichoonyeshwa na Yanga walipocheza nao kwenye mechi
ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara juzi Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.
Yanga na Ashanti ziliumana juzi ambapo
mabingwa hao watetezi waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 huku wakionyesha
kiwango cha chini tofauti na mashabiki walivyotegemea.
Kibadeni amesema mechi yao na Yanga ilikuwa nyepesi sana.
Alisema Yanga ya mzunguko wa kwanza
ilikuwa nzuri tofauti na hii ya sasa, ndiyo maana hata ushindi wao wameupata
kwa shida.
Aliongeza kuwa, kilichowafanya vijana
wake wapoteze mchezo huo ni kukosa umakini, pia kuna baadhi ya wachezaji wake walikuwa
wazito sana uwanjani na alipofanya mabadiliko ndipo wakafanikiwa kuwadhibiti
wapinzani wao na kuweza kupata bao hilo moja.
“Hawa Yanga mbona wepesi sana, wachezaji
wao wengi wanajiamini jambo ambalo katika mpira halitakiwi lakini nawapongeza
kwa kuwa wamepata pointi tatu na zitawasaidia, licha ya hivyo wasibweteke,”
alisema Kibadeni.
hizo mbwembwe tumezizoea kwa makocha wa kitanzania. Badala ya kuongea kiufundi wanaleta siasa na ndio maana hatusongi mbele
ReplyDelete