EYMAEL |
Pamoja na kukosa nafasi ya kuinoa Yanga
aliyokuwa akiitaka kwa udi na uvumba, imeelezwa Luc Eymael anaweza kupata
nafasi ya kuinoa timu ya taifa ya Rwanda.
Eymael raia wa Ubelgiji alikuwa kati ya
makocha wanaowaniwa kuinoa Yanga ambayo mwisho ilimnasa, Hans van Der Pluijm.
Mmoja wa rafiki wa karibu wameiambia
SALEHJEMBE, Eymael amekuwa kwenye mazungumzo wa na viongozi wa Shirikisho la
Soka la Rwanda (Ferwafa).
“Sijajua vizuri kama wanataka
akafundishe timu ya taifa au wanazungumza naye kwa niaba ya klabu fulani.
“Lakini najua watu wa Rwanda
wanamhitaji Eymael, tusubiri ndani ya siku mbili hizi tutajua,” alisema rafiki
yake huyo.
Eymael amewahi kuinoa AFC Leopards ya
Kenya na wakati anawaniwa na Yanga alikuwa kwao Ubelgiji.
0 COMMENTS:
Post a Comment