Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic
amesema ushindi kwa Rhino Rangers ya Tabora utakuwa bora kuliko wote
watakaopata kwenye Ligi Kuu Bara.
Logarusic raia wa Croatia amesema, kama
wataishinda Rhino, watakuwa na uhakika wa kujenga upya hali ya kujiamini na
kushinda mechi nyingine.
“Tunauhitaji ushindi wa Jumapili kupita
mwingine wowote, huo ndiyo utakaotupa dira tunakwenda wapi na nini cha kufanya.
“Kama tutashinda maana yake tunaweza
kujenga hali ya kujiamini na kujua cha kufanya.
“Wachezaji wanalijua hilo, ninawaamini
watafanya kila kitu kwa uhakika na kushinda mechi,” alisema Logarusic.
Simba inaanza kampeni za lala salama ya
Ligi Kuu Bara, kesho kwa kuivaa Rhino ya Tabora ambayo walitoka nayo sare ya
mabao 2-2 katika mzunguko wa kwanza.
0 COMMENTS:
Post a Comment