TALIB HILAL (KUSHOTO) AKIKABIDHI VIFAA KWA MWENYEKITI WA COASTAL UNION, AURORA. KATIKATI NI OFISA WA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI OMAN. |
Kocha wa timu ya taifa ya vijana ya ufukweni ya Oman, Talib Hilal
amesema kuwajali vijana ndiyo nguzo ya soka bora.
Akizungumza kutoka Oman, Hilal aliyewahi kukipiga Simba, amesema
mipango ya kuendeleza soka inaanza kwa vijana na lazima kila timu ilitilie
mkazo suala hilo.
“Mkiwa na msingi mzuri kwa vijana, lazima mnakuwa na uhakika wa
maendeleo katika soka.
“Hivyo lazima kuwapa nafasi vijana, wafundishwe na walimu bora,
watumie vifaa bora na wawekewe mazingira mazuri.
“Kama ni vipaji, Tanzania ina vipaji vingi sana na vinaweza
kufanya vizuri kama utaratibu utafuatwa,” alisema Talib.
Hivi karibuni, Talib alimwaga vifaa kwa timu ya vijana ya Coastal
Union ambayo ilishinda michuano ya Uhai Cup.
Hiyo ilikuwa ni mara ya pili kutoa msaada kwa timu ya vijana baada
ya kutoa vifaa kwa ile ya Simba, hata hivyo inaelezwa, havikufika.
0 COMMENTS:
Post a Comment