Maafande wa Ruvu Shooting wameshindwa
kuvunja rekodi ya Mbeya City ambayo haijafungwa hata mechi moja tokea kuanza
kwa Ligi Kuu Bara.
Katika mechi ya ligi hiyo leo kwenye
Uwanja wa Mabatini mjini Mlandizi, Pwani, timu hizo zimetoka sare ya bao 1-1.
Wenyeji ndiyo walianza kupata bao,
lakini Mbeya City wajaonyesha ni wabishi na kufanikiwa kusawazisha na ndiyo
yakawa matokeo hadi mwisho.
Awali Ruvu kupitia msemaji wao, Masau
Bwire walisema wangeivunja rekodi hiyo ya Mbeya City ambayo imekuwa ikipata
matokeo ya sare na ushindi tu.
0 COMMENTS:
Post a Comment