Robin van Persie ameonekana akijaza
mafuta ya kutosha kwenye gari lake.
Baada ya hapo akaingia na kutokomea
kusikojulikana, tayari hali hiyo imezua hofu, kwamba anakwenda wapi.
Taarifa zimekuwa zikieleza je, ni kweli
hana furaha? Na atataka kuondoka kabla ya dirisha la usajili linalofungwa leo
saa sita usiku.
Bado kuna maswali, maana Man United
imewapeleka kwa mkopo wachezaji wawili, Wilfred Zaha aliyetua Cardiff na
Anderson ambaye amekwenda Fiorentina hadi mwisho wa msimu.
Lakini imemuuza Fabio jumla kwa Cardiff,
je, itaongeza mtu zaidi ya Juan Mata iliyomnunua kutoka Chelsea kwa kitita cha
pauni milioni 37.1. tusubiri.
0 COMMENTS:
Post a Comment