January 22, 2014

TALIB (KUSHOTO) AKIKABIDHI VIFAA KWA AURORA.

Beki wa zamani wa Simba, Talib Hilal ametoa msaada wa vifaa kwa timu ya vijana ya Coastal Union iliyobeba ubingwa wa michuano ya Uhai Cup, hivi karibuni.



Talib ambaye sasa ni Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya ufukweni ya Oman, amekabidhi vifaa jezi seti mbili, seti ya fulana za mazoezi na mfuko wa kubebea mipira kwa uongozi wa Coastal Union.

Kocha huyo amekabidhi vifaa hivyo kwa Mwenyekiti wa Coastal Union, Aurora katika hafla iliyofanyika jijini Muscat, leo.

Hii ni mara kwanza kwa Hilal kutoa vifaa kwa timu ya vijana ya Coastal Union lakini mara ya kwanza kwa timu za Tanzania.

Msimu uliopita wakati Simba iliweka kambi jijini Muscat, Oman, Talib alikabidhi vifaa kama hivyo kwa uongozi wa Simba kwa ajili ya timu zao za vijana.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic