NIFANYEJE SASA? |
Mwakilishi wa kiungo Juan Mata
amesafiri hadi mjini Manchester kufanya mazungumzo ya mwisho ili atue na
kujiunga na United.
Tayari Chelsea imesema iko
tayari kumuachia kwa pauni milioni 37 na Man United inaonekana iko tayari
kuzitia.
Mata amekosekana mazoezi ya
Chelsea leo tena bila ya taarifa, hali inayoonyesha yuko katika harakati za
kujiunga na Man United.
Kocha Jose Mourinho wa Chelsea
anaonekana kupendelea kumtumia Oscar na William badala ya Mata ambaye ni kati
ya wachezaji wenye uwezo mkubwa wa kuengeneza nafasi.
Kuna taarifa, huenda Mata
akafanya vipimo vya afya usiku huu na tayari waandishi wa magazeti maarufu ya
Uingereza wanamwinda kwa juhudi.
Mmoja wa mtandao umeandika
ndani ya saa mbili hadi tatu, jibu litakuwa limepatikana lakini hakuna
uthibitisho kwa asilimia mia hadi sasa.
0 COMMENTS:
Post a Comment