Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesogeza mbele mechi za raundi ya 14 na 15 zinazoihusu timu ya Tanzania Prisons zilizokuwa zichezwe Januari 25 na 29 mwaka huu.
Awali Tanzania Prisons ilitakiwa kutafuta uwanja mwingine wa kuchezea mechi hizo dhidi ya Ruvu Shooting na JKT Ruvu kutokana na Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine kutokuwa tayari kwa Ligi Kuu ya Vodacom wikiendi hii.
Mechi hizo sasa zitachezwa kati ya Februari 6 na 8 mwaka huu kwenye uwanja huo huo wa Kumbukumbu ya Sokoine.
0 COMMENTS:
Post a Comment