CHEKA AKIMTWANGA MMAREKANI NA KUTWAA MKANDA JIJINI DAR |
Bondia Francis Cheka amefunguka kuwa,
njaa ndiyo iliyosababisha apokonywe mkanda wake wa WBF kwa kuwa alikuwa hana
jinsi ndiyo maana alikwenda kupigana nje ya nchi.
Cheka alipokonywa mkanda wake wa WBF
kwa kupigwa kwa KO na Mrusi, Fedor Chudinor alipokwenda kucheza kwenye Ukumbi
wa Dynamo Palace of Sports, Krylatskoye, Urusi, Desemba, mwaka jana.
Cheka alisema njaa ndiyo iliyomfanya
aende kupigana nchini humo kwa kuwa hakuwa na fedha, kwani hata yeye mwenyewe
aliona hana uwezo wa kumpiga bondia huyo kutokana na maandalizi hafifu
aliyoyafanya.
“Sikuwa na maandalizi mazuri,
nilikosa fedha, hali iliyosababisha niuze mifuko yangu ya simenti na matofali
ndiyo nifanikiwe kwenda kupigana. Kwa kifupi njaa ndiyo iliyonipeleka kule,
sikuwa na maandalizi,” alisema Cheka.
Bondia huyo ndiye bora zaidi kwa
kipindi hiki lakini amekuwa akilalamika malipo kidogo anayoyapata kutoka kwa
mapromota yanapunguza kasi ya maendeleo yake.
0 COMMENTS:
Post a Comment