Aliyekuwa Kocha Msaidizi wa Yanga,
Fred Felix Minziro, amesema yupo tayari kurudi kuifundisha timu hiyo muda
wowote endapo uongozi wa klabu hiyo utahitaji huduma yake, licha ya kumtimua
hivi karibuni.
Uongozi wa Yanga uliwatimua Minziro
pamoja na makocha wenzake, Ernie Brandts aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo na
Razack Siwa aliyekuwa kocha msaidizi, kutokana na kutoridhishwa na utendaji wao
wa kazi.
Minziro amesema licha ya kutimuliwa
na Yanga, bado ana mapenzi ya dhati na timu hiyo na endapo uongozi utahitaji
huduma yake, basi atarejea kuendelea na kazi yake hiyo.
Alisema hana kinyongo na viongozi wa
timu hiyo, licha ya maamuzi makali waliyoyachukua dhidi yake na kwamba
ameyapokea kwa mikono miwili.
"Hivi sasa nahitaji kupumzika
kwanza kwa sababu timu zote za ligi kuu zina makocha wao, labda nitaanza
harakati za kutafuta kazi mwishoni mwa msimu huu.
"Hata hivyo kama uongozi wa
Yanga utahitaji huduma yangu kwa mara nyingine, basi mimi nipo tayari kurudi
kwa sababu nina mapenzi ya dhati na klabu hiyo," alisema Minziro.
0 COMMENTS:
Post a Comment