January 31, 2014


Kocha wa makipa wa Yanga, Juma Pondamali, wikiendi iliyopita alitoa kali katika mechi dhidi ya Ashanti United kwenye Uwanja wa Taifa, Dar baada ya kuingia uwanjani kisha kufundisha huku akiwa na vifaa vya kusikilizia muziki ‘headphones’.


Katika mechi hiyo ambayo Yanga ilipata ushindi wa mabao 2-1, Pondamali alivaa headphones hizo shingoni huku akiendelea na majukumu yake kama kawaida.

Pondamali alionekana kuwa na vifaa hivyo wakati wa mazoezi ya kuwapasha misuli huku akitoa maelekezo makipa wake, hata baada ya mechi kuanza bado alikuwa amezivaa, aliendelea kuwa nazo mpaka mwisho wa mechi.

Alipoulizwa alisema: “Kweli nilikuwa nimezivaa niliogopa kuziacha vyumbani kwa kuwa zinaweza kupotea nanikakosa wa kumlaumu. Lakini kwa kuwa nilikuwa sisikilizi muziki sikuona tatizo lolote.


“Nitazivaa pia hata katika mechi ya Coastal kwa kuwa haziniharibii chochote,” alisema Pondamali. Lakini katika mechi ya juzi dhidi ya Coastal, hakuzivaa, badala yake alikuwa amevaa kofia ‘cap’ huku ameigeuza nyuma.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic