Kocha Mkuu wa Coastal Union, Yusufu Chippo amedai kuwa msimu huu Azam FC ndiyo
mabingwa wa Ligi Kuu Bara.
Chippo amesema endapo hautafanyika ujanjaujanja, Azam
ndiyo itakuwa bingwa wa Tanzania Bara.
“(Coastal)
Hatuna tena nafasi ya kupigania ubingwa, ila tuna nafasi ya kuhakikisha
tunamaliza ligi hiyo tukiwa pazuri zaidi.
“Timu
ambayo msimu huu inaweza kutwaa ubingwa huo ni Azam, nasema hivyo kwa sababu
ina kila kitu ambacho kinaweza kuifanya ifikie hatua hiyo bila kuwa na tatizo
lolote kuanzia uimara wa kikosi chake hadi kiuchumi,” alisema Chippo.
Azam
inaongoza msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 33 ikifuatiwa na Yanga yenye
pointi 32 huku Mbeya City ikishika nafasi ya tatu ikiwa na 31.
0 COMMENTS:
Post a Comment