Kiungo Hassan Dilunga amepata nafuu
baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa malaria akiwa nchini Uturuki.
Dilunga yuko na Yanga nchini humo katika
kambi ya wiki mbili kujiandaa na Ligi Kuu Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.
Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto amesema
Dilunga yuko katika hali nzuri ukilinganisha na jana na juzi.
“Sasa anaendelea vizuri kabisa, naweza
kusema amepona ukilinganisha na siku mbili zilizopita,” alisema Kizuguto.
Aidha, Kizuguto pia alikamatwa na
malaria, hata hivyo ameeleza kumaliza dozi na hali yake ni nzuri pia.
0 COMMENTS:
Post a Comment