Nahodha na beki wa pembeni wa Simba,
Said Nassor ‘Chollo’, amelazimika kupumzishwa kwenye timu hiyo kwa ajili ya
kupisha matibabu anayofanyiwa kwa sasa.
Chollo aliyekumbwa na majeraha mfululizo
ndani ya kipindi kifupi, ameanza matibabu mara baada ya vipimo vilivyofanyika
Ijumaa katika hospitali inayofahamika kwa jina la Doctors Plaza iliyopo Upanga,
Dar kuonyesha kuwa ana tatizo kwenye nyonga yake ya kushoto.
Ofisa
Habari wa Simba, Asha Muhaji, alisema matibabu hayo yatachukua wiki tatu.
Alisema kuwa beki huyo atakapomaliza
matibabu hayo, atahitajika kuchukuliwa tena vipimo vya kina kwa ajili ya
kujiridhisha kama tatizo hilo litakuwa limekwisha au la.
“Kwa sasa Chollo atakaa nje ya uwanja
kwa muda wa wiki tatu akiendelea na matibabu huku akihitajika kuhudhuria
hospitalini mara kwa mara ndani ya muda huo ambapo kwa mujibu wa madaktari
waliomtibu, muda huo ukimalizika, atafanyiwa tena vipimo kuangalia tatizo kama
litakuwa limekwisha,” alisema Muhaji.
0 COMMENTS:
Post a Comment