Kiungo aliyesimamishwa kwa muda usiojulikana na klabu yake ya Yanga, Athumani Idd
‘Chuji’, jana asubuhi alikabidhi barua ya kuomba radhi kwa uongozi wa klabu
hiyo iliyopo Mtaa wa Jangwani.
Moja wa viongozi wa klabu hiyo ambaye aliomba jina lake lihifadhiwie kutokana na yeye kuwa si msemaji wa klabu hiyo alisema kuwa majira ya saa tano asubuhi Chuji alifika klabuni na kukabidhi barua hiyo ambayo inamaelezo ndani yake ya kuomba radhi.
“Chuji
alikuja asubuhi akaonana na baadhi ya viongozi wa klabu na kukabidhi barua hiyo
lakini kuhusu kumsamehe au kutomsamehe jukumu lote ameachiwa (Abdallah) Bin
Kleb,” alisema kiongozi huyo.
Chuji
hakupokea simu yake wakati Bin Kleb hakupatikana kulizungumzia hilo.
0 COMMENTS:
Post a Comment