Makipa wa Yanga wamevimba
nyonga ‘hips’ kutokana na mazoezi makali ambayo wamekuwa wakipewa na kocha wao
wa makipa, Juma Pondamali.
Makipa hao ni Juma
Kaseja, Ally Mustafa ‘Barthez’, Deogratius Munishi ‘Dida’ na Yusuf Abdul.
SALEHJEMBE ilishuhudia makipa wote wakilalamika kuvimba nyonga kutokana na mazoezi ya
Pondamali.
Alipoulizwa Pondamali juu
ya hilo, alisema: “Makipa wangu wanalalamika sana wamevimba hips kutokana na
mazoezi ninayowapa, ni kweli lakini wajue hapo nawaongezea uwezo zaidi na
nitaongeza,” alisema Pondamali.
Wakati huohuo, kabla ya
kuondoka, Yanga ilikuwa ikifanya mazoezi kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers,
Kawe jijini Dar ambapo pembeni kidogo na walipokuwa wakifanya mazoezi kulikuwa
na kinyesi cha ng’ombe.
0 COMMENTS:
Post a Comment