Timu ya Coastal Union inatarajiwa
kurejea nchini kesho, huku ikiahidi kufanya mambo makubwa kwenye Ligi Kuu
Tanzania Bara mzunguko wa pili.
Coastal ipo nchini Oman kwa wiki mbili
kwa ajili ya kujiandaa na mzunguko huo wa pili wa ligi kuu, ikiwa chini ya
kocha wao mpya, Yusuph Chippo.
Mwenyekiti wa timu hiyo, Mohamed Aurora, alisema timu hiyo inarejea ikiwa na matumaini ya kuanza vyema katika ligi kutokana na maandalizi waliyofanya huko.
Aurora alisema wamejifunza mengi
walipokuwa huko na wamecheza mechi za kirafiki na timu za ligi kuu na moja ya Ligi
Daraja la Pili ambazo zimeweza kuwajenga kwa kiasi kikubwa na kuwa imara zaidi.
“Timu itarejea nchini ikiwa na matumaini
ya kufanya vyema kutokana na maandalizi
tuliyoweza kufanya huku. Ilifika kipindi
tulibadili muda wa mazoezi ili kuendana
na hali ya hewa ya kwetu.
“Lakini kikubwa tunashukuru mipango na
malengo yetu yamekwenda vizuri na ninaamini katika mzunguko huu wa pili,
Coastal itakuwa nyingine kutokana na mabadiliko
ambayo yametokana na maandalizi tuliyofanya huko ili kuweza kuwa katika
nafasi nzuri,” alisema Aurora.
Coastal ilimaliza mzunguko wa kwanza
ikiwa katika nafasi ya nane na pointi 16.
0 COMMENTS:
Post a Comment