Maandalizi
ya mbio za 12 za Kilimanjaro Marathon zinazotarajiwa kufanyika Machi 2, 2014
huko Moshi yanaendelea kushika kasi baada ya waandaaji wa mbio hizo kutangaza
ada za ushiriki pamoja na ratiba ya mbio hizo.
John
Addison, Mkurugenzi Mkuu wa Wild Frontiers, waandaaji wa mbio hizo alisema
katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana kwamba mbio ndefu za 42km
Kilimanjaro Premium Lager Marathon zitaanza saa 12:30 asubuhi huku mbio za 10km
Gapco Disabled Marathon zikianza saa 12:45 asubuhi, Nusu Marathon km 21 saa 1
kamili asubuhi na mbio za kujifurahisha za Vodacom 5km Fun Run zitaanza saa
moja na robo asubuhi. Alisema ratiba hii imepangwa kwa mtiririko huu ili kuwapa
fursa washiriki wa kila mbio kuona mandhari ya mji wa Moshi na Mlima
Kilimanjaro.
Alisema
kuwa viingilio vya mbio ndefu za Full Marathon km 42 viingilio itakuwa ni dola
60 kwa washiriki wa kimataifa, Tsh 6,000 kwa raia wa Afrika Mashariki na dola
30 kwa raia wa kigeni wanaoishi au kufanya kazi Afrika Mashariki wakati huku
Nusu Marathon viingilio ikiwa ni dola 60 kwa washiriki wa kimataifa, shilingi
4,000 kwa raia wa Afrika Mashariki na dola 30 raia wa kigeni wanaoishi Afrika
Mashariki
Aidha,
washiriki wa kimataifa kwenye mbio za walemavu za GAPCO watalipia dola 10,
shilingi 3,000 kwa raia wa Afrika Mashariki na dola tano kwa raia wa kigeni
wanaoishi Afrika Mashariki. Mbio hizo za walemavu zitahusisha shindano la mbio
za kutumia baiskeli za mikono (Handcycle) na viti vyenye magurudumu
(Wheelchair) tu. Washiriki wa kimataifa na raia wa kigeni waishio Afrika
Mashariki watalipa dola mbili na raia wa Afrika Mashariki watalipa shilingi
3,000 mbio za kujifurahisha za Vodacom 5km Fun Run.
Kwa
mujibu wa Addison, umri wa kushiriki mbio za kilomita 42 ni miaka 21, miaka 18
kwa nusu marathon na mbio za walemavu huku kwenye mbio za kujifurahisha ikiwa
ni miaka kumi. “Tutasajili washiriki kwa muda wa siku mbili kabla ya mbio
ambapo kwenye hoteli ya Keys Hotel mjini Moshi tarehe 28 Februari na tarehe 1
Machi kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa 11 jioni kila siku na pia uandikishwaji
utafanyika Arusha tarehe 27 Februari katika eneo ambalo litatangazwa badae,”
alisema.
Mbio
hizo zinadhaniwa kuwa kati ya mbio kubwa zaidi duniani za kitalii na ndio tukio
kubwa zaidi la kimichezo Tanzania. Kilimanjaro Marathon ya mwaka huu
inatarajiwa kuwa na washiriki zaidi ya 6,000 wakiwemo takribani wageni 600
kutoka nchi zaidi ya 40.
Kilimanjaro
Marathon 2014 inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager (wadhamini wakuu),
Vodacom Tanzania (5km Fun Run), GAPCO (10km Disabled Run), FNB Tanzania, TPC
Sugar, Simba Cement, KK Security, Kilimanjaro Water, Keys Hotel, TanzaniteOne
na UNFPA.
0 COMMENTS:
Post a Comment