Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amesema shirikisho lake limepanga malengo ya muda
mfupi na mrefu ikiwa na sehemu ya mkakati wa kuendeleza na kuinua kiwango cha
mchezo huo nchini.
Malinzi ameeleza mikakati hiyo ya
uongozi wake leo (Januari 20 mwaka huu) wakati alipomtembelea Waziri Mkuu wa
zamani Edward Lowassa ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Amesema uongozi wake umepanga malengo
hayo ikiwemo kuandaa mashindano maalumu ya kutafuta vipaji mikoani ili kuondokana
na mtindo wa timu ya Taifa (Taifa Stars) kuundwa na wachezaji kutoka katika
klabu chache tu.
Kwa upande wake Lowassa ambaye pia ni
Mbunge wa Monduli ameelezea matumaini yake kwa uongozi mpya wa TFF katika
kuunga mkono juhudi za Rais Jakaya Kikwete katika kuimarisha na kuinyayua
Tanzania katika ramani ya mpira wa miguu duniani.
0 COMMENTS:
Post a Comment