January 31, 2014

DILUNGA
Wakati timu yake ya Yanga ikiumana na Coastal Union jijini Tanga, juzi Jumatano, kiungo wa klabu hiyo ya Jangwani, Hassan Dilunga, alitua kwenye Uwanja wa Mabatini kuwashuhudia Ruvu Shooting wakicheza dhidi ya Mbeya City.


Dilunga ambaye amejiunga na Yanga kwenye usajili wa dirisha dogo msimu huu akitokea Ruvu Shooting, alionekana kuwa mwenye furaha huku akitaniana na wachezaji wa Ruvu pindi walipopata nafasi, ambapo wapo waliomwambia karibu nyumbani.

Championi Ijumaa lilimshuhudia nyota huyo akishuhudia mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Mabatini huku mashabiki wa Ruvu wakimshangilia na kumwambia karibu nyumbani pia.


Dilunga aliifuatilia mechi hiyo kwa umakini mkubwa ambapo inaelezwa kuwa, hajaenda Tanga kwa kuwa anasumbuliwa na homa ya matumbo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic