Mashabiki wa soka mkoani hapa wamembandika
jina jipya Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm kwa kumuita Capello,
wakimfananisha na kocha wa zamani wa Juventus, Fabio Capello.
Mara baada ya Pluijm kuingia uwanjani na
kuanza kuwasalimu mashabiki wa timu hiyo, walimshangilia huku wengine wakimwita
Capello, kocha ambaye sasa anakiongoza kikosi cha Urusi.
Baada ya kumalizika kwa mchezo huo, SALEHJEMBE iliwahoji mashabiki hao juu ya sababu za kumpa jina hilo ambapo
walisema kuwa eti amefanana na Capello.
“Jamaa anafanana sana na Capello,” alisema
shabiki mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Juma Hassan lakini kabla
hajamaliza, mwingine aliyejitambulisha kama Ramadhan Athumani, akadakia: “Ila
wanatofautiana kidogo sana kwa sababu huyu ana kitambi lakini Capello hana.”
0 COMMENTS:
Post a Comment