Hali ya
ushindani wa kufunga mabao kwa mastraika wa Ligi Kuu Bara inazidi kupamba moto
baada ya Kipre Tchetche wa Azam kufikisha mabao tisa ikiwa ni tofauti ya bao
moja na kinara Amissi Tambwe wa Simba mwenye 10.
Tambwe amesema kuwa hajawahi kumuona Tchetche hata siku
moja lakini kutokana na taarifa anazozisikia, anaamini kuwa ni straika mzuri
ila akaahidi kupambana naye.
Alisema
kuwa hali kama hiyo hutokea kwenye ligi yoyote yenye ushindani lakini ameupokea
ushindani huo kwa mikono miwili na anaamini atafunga mabao mengi zaidi kwenye
mechi zijazo.
“Ni hali
nzuri ya ushindani na inaonyesha kuwa ni straika mzuri kutokana na spidi yake
lakini na mimi pia nitafunga kama kawaida kila ninapopata nafasi ili niongeze
idadi kubwa na mwisho wa msimu niweze kutwaa ufungaji bora,” alisema Tambwe.
Kwa
matokeo hayo, Tchetche sasa amekwea mpaka nafasi ya pili akifungana na Elias
Maguri wa Ruvu Shooting wakifuatiwa na Juma Luizio wa Mtibwa na Hamis Kiiza wa
Yanga wenye mabao nane kila mmoja.
0 COMMENTS:
Post a Comment