Mshambuliaji wa kimataifa wa Yanga, Emmanuel
Okwi, amesema kambi ya timu hiyo inayotarajiwa kupigwa nchini Uturuki,
itakibadilisha kwa kiasi kikubwa kikosi hicho na kukifanya kitetee ubingwa wake
msimu huu.
Yanga ambayo ni bingwa mtetezi,
inaongoza ligi ikiwa na pointi 28 na inatarajiwa kwenda Uturuki kesho Alhamisi
kuweka kambi ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.
Akizungumza na Championi Jumatano, Okwi
aliyejiunga na Yanga akitokea Sports Club Villa ya Uganda, alisema mpaka sasa
wachezaji hawazajazoeana, hivyo anaamini wakiwa huko mwalimu atatengeneza
kombinesheni nzuri itakayoleta matunda katika timu hiyo.
Alisema anaomba sapoti kwa mashabiki ili
waweze kufanikisha lengo lao la kutwaa ubingwa kwa mara ya pili mfululizo kwa
kuwa hilo linawezekana iwapo tu watakuwa kitu kimoja.
“Nafurahia sana kwa kuwa kambi inakuja wakati
muafaka, itatusaidia kuimarisha kikosi chetu kwani kama unavyojua wachezaji
wengine bado wapya, hivyo wanahitaji utulivu kujuana na kutengeneza
kombinesheni nzuri.
“Ukweli naamini kuwa sapoti ya mashabiki
wa Yanga inaweza kutufanya tukawa mabingwa msimu huu, hili ndiyo jambo zuri
kwetu,” alisema Okwi.
0 COMMENTS:
Post a Comment