Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie
Brandts ameushukuru uongozi wa Yanga na wadau wote waliomuunga mkono.
Brandts, beki wa zamani wa Roda JC na
timu ya taifa ya Uholanzi amesema anaushukuru uongozi huo wa Jangwani pamoja na
wadau wote wa soka, lakini pia mashabiki wa Yanga.
“Nafikiri nitaondoka ndani ya siku mbili
kurejea nyumbani, muda wangu hapa umeisha. Acha niende, lakini nawashukuru
sana.
“Uongozi hata kama kulikuwa na kasoro,
lakini wadau mbalimbali na mashabiki wa Yanga ambao walikuwa muhimu sana.
“Waambie wachezaji nawatakia kila la
kheri na kuna wale waliokuwa na matatizo, basi warekebishe ili kuendelea
kuisaidia Yanga,” alisema.
Brandts aliingoza Yanga kutwaa ubingwa
wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita.
Wakati uongozi unamfukuza kikosi chake
ndiyo kinachoongoza ligi hadi mzunguko wa kwanza ulipofikia mwisho.
Yanga ilimfukuza baada ya kufungwa kwa
mabao 3-1 dhidi ya Simba katika mechi ya kirafiki ya Nani Mtani Jembe.
Hata hivyo wadau wamekuwa wakilalamika
kwamba si sahihi kwa kuwa kocha kama yeye hapaswi kufukuzwa kwa mechi ya
kirafiki.
0 COMMENTS:
Post a Comment