Simba imemaliza siku vizuri leo kwa
kufanikiwa kufuzu kucheza robo fainali ya michuano ya Mapinduzi.
Simba imefuzu baada ya kuwachapa KMKM ya
Zanzibar kwa bao 1-0 lililofungwa na mkongwe Amri Kiemba maarufu kama Baba
Shabani.
Bao hilo lilifungwa katika dakika ya 6
baada ya Kiemba kuruka na kuunganisha kwa kichwa krosi krosi safi ya Ali Badru.
Kwa mara ya kwanza Kocha Mkuu, Zdravko
Logarusic alikuwa amerejea kwenye benchi la timu hiyo.
Awali Simba iliongozwa mechi mbili za
mwanzo na kocha wake msaidizi, Selemani Matola.
Kikosi kamili cha Simba kilipangwa hivi:
Yaw Berko, William
Lucian ‘Gallas’, Omar Salum/Miraj Athumani, Gilbert Kaze ‘Demunga’, Donald
Mosoti/Joseph Owino, Abdulhalim Humud, Uhuru Selemani/Said Ndemla, Amri Kiemba,
Betram Mwombeki/Zahor Pazi, Ali Badru na Edward Chistopher/Adeyum Saleh.
Kikosi cha KMKM; Mudathir Khamis, Pandu Hajji, Haidhurun Juma, Khamis Ali, Iddi Kambi, Ibrahim Khatibu, Nassor Omar/Hajji Simba, Maulid Kapenta, Vincent Kamanya na Machano Abdallah.
0 COMMENTS:
Post a Comment