Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko
Logarusic amesema kikosi chake kutwaa Kombe la Mapinduzi si ishu kubwa sana
kwake.
Logarusic ambaye ameungana na Simba
akitokea kwao Croatia amesema ataitumia michuano hiyo kama sehemu ya kuboresha
kikosi hicho
“Tunacholenga sisi ni Ligi Kuu Bara.
Michuano hii ni kama ya kirafiki, tunaweza kuchukua au kutochukua ubingwa na
haitakuwa ishu kubwa sana.
“Nataka kutengeneza kikosi changu
vizuri zaidi ndiyo maana niliamua kuwa wachezaji ambao hawakupata nafasi katika
mechi dhidi ya Yanga, watapata nafasi huku Zanzibar,” alisema Logarusic.
Kocha huyo alisisitiza wachezaji
watatakiwa kumuonyesha kwamba wanaweza kila atakapowapa nafasi la sivyo
watapoteza kabisa sifa ya kuwa katika kikosi chake.
Jana wakati Simba inaivaa KMKM,
Logarusic alisema kipa Yaw Berko na kiungo Abdulhalim Humud ni kati ya
watakaopata namba.
0 COMMENTS:
Post a Comment