January 12, 2014



 
MKWASA (KULIA) AKIWA UTURUKI NA ROBERTO CARLOS NA KIUNGO WAKE NIZAR KHALFAN
Kocha Msaidizi wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa analazimika kurejea nyumbani jijini Dar es Salaam na kuiacha Yanga ikiendelea na mazoezi mjini Antalya, Uturuki.


Mkwasa ambaye amesafiri na Yanga iliyoweka kambi nchini humo atatua nchini Ijumaa ili kushughulikia masuala yanayohusiana na ndoa yake.

Hata hivyo Mkwasa atalazimika kusubiri hadi Kocha Mkuu mpya, Hans van Der Pluijm ajiunge na kikosi hicho.

Yanga inaingia naye mkataba wa miaka miwili na ataondoka keshokutwa Jumanne kwenda Uturuki wakati kesho anataka kwenda Zanzibar kuiona Simba ya Zdravko Logarusic ikicheza fainali ya Kombe la Mapinduzi.
 
Mkwasa ni mme wa Mkuu wa Wilaya wa Bahi, Betty Mkwasa na kurudi kwake ni kwa ajili ya sherehe yao ya kusherekea zaidi ya miaka 20 ya ndoa yao.

Mkwasa amejiunga na Yanga akitokea Ruvu Shooting alikokuwa kocha mkuu na sasa anaitumikia Yanga katika nafasi ya kocha msaidizi.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Yanga zinaeleza, uongozi umelazimika kumpa Mkwasa ruhusa hiyo kwa kuwa alikuwa na mipango hata kabla ya kuajiliwa.

“Mkwasa alikuwa mkweli kabla ya kuajiliwa, ilikuwa ni uongozi uangalie suala hilo maana aliliweka mezani mapema na lazima asherekee.

“Kwa hiyo uongozi ukakubali, kikosi kizima kitarejea nchini Januari 22, lakini Mkwasa analazimika kurudi mapema, nafikiri ni Januari 17,” kilieleza chanzo cha uhakika.
Tayari Mkwasa ameiongoza Yanga kushinda mechi ya kwanza ya kirafiki kwa mabao 3-0, mechi hiyo ilipigwa juzi katikia Uwanja wa Hoteli ya Sueno Beach Side nje kidogo ya mji wa Antalya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic