Ghana imetinga fainali ya Kombe la Chan na sasa itacheza na Libya
katika mechi itakayopigwa Jumamosi jijini Cape Town, Afrika Kusini.
Ghana imetinga fainali kwa kuifunga Nigeria kwa mikwaju 4-2 ya penalti
katika mechi iliyomalizika punde katika Uwanja wa Mangaung.
Mechi kati ya timu hizo za Afrika Magharibi ilikuwa kali na ya kuvutia
lakini kila upande ulipoteza nafasi kadhaa.
Kabla ya mechi hiyo, Libya pia ilivuka kwa mikwaju ya penalti
dhidi ya Zimbabwe na inaonyesha fainali itakuwa ngumu kutokana na uimara wa
vikosi hivyo.
MATOKEO MENGINE KUANZIA MWANZO HADI KABLA YA FAINALI
0 COMMENTS:
Post a Comment