Man City imetoa dozi ya mabao 5-1 kwa Tottenham katika mechi
iliyomalizika hivi punde huku Chelsea nayo ikilazimishwa sare tasa dhidi ya
West Ham United.
Ushindi huo unaifanya City irejee kileleni mwa Ligi Kuu England
kwa pointi 53, ikiishuka Arsenal yenye 52 hadi katika nafasi ya pili wakati
Chelsea inabaki katika nafasi ya tatu na pointi 50.
Mechi hizo mbili za Ligi Kuu England zilikuwa na mvuto mkubwa na
ilionekana kama Spurs itaisumbua City lakini taratibu ilianza kuruhusu nyavu
zake kutikiswa.
0 COMMENTS:
Post a Comment