Kipa wa Mtibwa Sugar,
Said Mohamed, amesema kuwa ana mpango wa kwenda kucheza soka nchini Vietnam
mara baada ya kumalizika kwa msimu huu ikiwa ni kutokana na kupata mwaliko wa
kwenda nchini humo.
Said ambaye ametua
klabuni hapo msimu huu baada ya kukosa namba katika kikosi cha Yanga, pia
amekosa nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza cha Mtibwa.
“Baada ya mzunguko wa
pili kumalizika, natarajia kwenda nchini Vietnam kwa ajili ya majaribio,
nimepata mwaliko.
“Malengo yangu kwa sasa
ni kuhakikisha napata nafasi kikosi cha kwanza hapa Mtibwa ili kuwa kwenye
kiwango kizuri kabla ya kwenda,” alisema Said.
SOURCE: CHAMPIONI
0 COMMENTS:
Post a Comment