Beki wa kati wa Ashanti United, Victor Costa ameionya na kuipa mbinu Azam FC ambayo
itavaana na Ferroviario da Beira ya Msumbiji katika hatua ya awali ya Kombe la
Shirikisho Afrika inayotarajiwa kutimua vumbi Februari, mwaka huu.
Costa
ambaye aliwahi kucheza soka la kulipwa nchini Msumbiji, amesema iwapo Azam
inahitaji kusonga mbele zaidi katika michuano hiyo, inatakiwa ijipange vizuri
kwa kuwa wapinzani wao hao wapo kamili.
“Ferroviario
ni nzuri, nawajua hao jamaa, Azam wanatakiwa wasiidharau, hivyo siri kubwa ni
kuhakikisha wanaingia wakijua wanakutana na timu ngumu la sivyo yatakuwa
mengine.
“Sijui
kuna mabadiliko gani ya ziada katika timu hiyo, maana ni muda mrefu tangu
nilivyoondoka, lakini naamini bado wapo vizuri, cha msingi ni kujiandaa tu,”
alisema Costa.
0 COMMENTS:
Post a Comment