Mshambulaiji wa JKT Ruvu, Paul Ndauka, wiki iliyopita alikutana na changamoto kubwa kwenye
Mtandao wa Kijamii wa Facebook, baada ya kuandika ujumbe wa kumtetea kiungo wa
Yanga, Athuman Idd ‘Chuji’.
Mshambuliaji
huyo aliandika ujumbe wa kumtetea kiungo huyo na kuwataka watu waache
kumfuatafuata kwa kuwa anajua alifanyalo.
Chuji kwa
sasa amesimamishwa klabuni kwake kwa muda usiojulikana kutokana na utovu wa
nidhamu.
Kiungo
huyo aliandika: “Kila mtu Chuji kazingua, vipi jamani mbona siyo kiivyo? Acheni
kumfanya Chuji kama kaua na hakuna binadamu ambaye hakosei.
“Sema
wewe umekosea mara ngapi na watu wakakusamehe, makosa mengine yanaongezewa
majungu na watu kama Kibadeni na flaniflani ambao hujiona magwiji wa mpira wa
Bongo…”
Wengi waliochangia
walionekana kuwa tofauti na Ndauka ambapo wapo waliofikia hatua ya kumtolea
lugha kali na kumtaka kutoingilia maamuzi ya uongozi wa Yanga.
0 COMMENTS:
Post a Comment