January 20, 2014

KIKOSI CHA MTIBWA SUGAR
Beki wa Mtibwa Sugar, Salim Mbonde, juzi Jumamosi alizimia katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na sasa amepewa siku tatu za kupumzika.


Mbonde alizimia kwa dakika tano baada ya kugongwa na kipa wa timu yake Hussein Sharifu ‘Casillas’ na straika wa Simba, Betram Mwombeki wakati akiokoa mpira uliokuwa umepigwa golini kwake.

 Mbonde amesema daktari wa kikosi hicho chenye maskani yake Manungu, amempa siku tatu kwa ajili ya kumtazama kama amepona kabisa.

Alisema binafsi anajisikia vizuri na anamshukuru Mungu kwa kuwa mzima mpaka sasa na anachukulia tukio hilo kama sehemu ya mchezo.

“Nimepewa siku tatu za mapumziko, baada ya hapo daktari ataniangalia tena, akiona nimekaa sawa ndiyo ataniruhusu.

“Unajua siku ile (juzi) wakati nafanyiwa hivyo nilikuwa naokoa mpira uliokuwa umepigwa golini kwetu, sasa wakati naruka juu nikakutana na Mwombeki na Casillas, wakanigona, baada ya hapo sikuelewa kitu hadi niliposhtukia nipo kwenye geti la kuingilia uwanjani napelekwa maabara,” alisema Mbonde.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic