MGOSI WAKATI AKIWA SIMBA |
Mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Mussa Mgosi, juzi alikuwa kivutio kikubwa baada ya kukaa
benchi na mtoto wake wa kike wakati mechi ikiendelea, akiwa ni mmoja wa wachezaji wa akiba ‘sub’.
Ilikuwa
ni katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Simba uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam. Simba ilifungwa 1-0.
Championi
lilimshuhudia mshambuliaji huyo akiwa na binti yake katika benchi ambalo
wachezaji wa akiba hukaa pamoja na makocha wao.
Mgosi
hakucheza kabisa mchezo huo na muda mwingi alikuwa karibu na mtoto wake huyo
anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka mitatu au minne.
Hata
baada ya mchezo huo, mtoto huyo aliendelea kuwa bega kwa bega na baba yake na
kila kona aliyopita, alikuwa naye hata alipokuwa akifanya mahojiano na
waandishi wa habari.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Mgosi alisema: “Binti
wangu huyu alipenda siku ya leo niongozane naye na hata alipokuja uwanjani
alinifuata na sikuona kama ni tatizo.”
0 COMMENTS:
Post a Comment