Mbeya
City ipo tayari kuanza mazungumzo ya awali na kipa raia wa DR Congo, Ikolonga
Type, lakini zoezi hilo limeshindikana baada ya kutokuwepo nchini kwa beki
kiraka wa Yanga, raia wa Rwanda, mwenye asili ya Congo, Mbuyu Twite.
Imeelezwa
kuwa, Mbeya City walianza kumfuatilia kipa huyo tangu walipouona uwezo wake
alipokuwa akifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Leaders uliopo Kinondoni, Dar.
Rafiki wa
karibu na mchezaji huyo ameiambia SALEHJEMBE kuwa kipa huyo ameshindwa
kufanya maamuzi akimsubiri Twite arudi kutoka Uturuki alikoenda kuweka kambi na
Yanga kwa kuwa ndiye mwenyeji wake hapa Tanzania.
“Alimuona
Type pale Leaders akamfuata akataka kuzungumza naye kuhusu usajili wa msimu
ujao lakini yeye hakuwa tayari akamwambia tusubiri Twite arudi ndiyo mambo
mengine yatafuata kuhusu usajili wake,” kilisema chanzo hicho.
Alipotafutwa
Type alisema: “Ni kweli kuna kiongozi nimezungumza naye kuhusu Mbeya City
lakini namsubiri kwanza Twite.” Mbuyu anatarajiwa kutua nchini alfajiri ya leo
kutoka Uturuki.
0 COMMENTS:
Post a Comment