Gumzo la beki Shomari Kapombe kushindwa kwenda nchini Ufaransa kuendelea na kazi katika timu yake ya daraja la nne linazidi kuchukua sura mpya kila kukicha.
Imeelezwa
kuwa Kapombe ambaye alirejea nchini kuitumikia Taifa Stars, Desemba, mwaka jana,
kisha kukwama kurudi Ufaransa, alipanda ndege kwa ajili ya kuelekea nchini humo
lakini alipofika Nairobi nchini Kenya, akashushwa, kisha akarejeshwa Tanzania.
Safari ya
Kapombe ilikuwa ni kurejea kwenye klabu yake ya AS Cannes inayoshiriki Ligi
Daraja la Nne Ufaransa lakini kutokana na visa yake kuwa na matatizo,
akalazimika kuishia Nairobi na kurudi jijini Dar es Salaam ambako ndiko alipo
mpaka sasa.
Akizungumza
na Championi Ijumaa, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),
Boniface Wambura alisema baada ya wao kumfanyia mipango yote ya kusafiri kwenda
Ufaransa, safari ikaanzia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius
Nyerere jijini Dar.
“Mara ya
kwanza alichelewa ndege, hivyo tukaamua kumkatia nyingine, ambapo alipofika
Nairobi alikwama kwa muda kutokana na visa yake kuonekana ina matatizo, ikabidi
arudi huku (Dar) ambapo ikabidi tumfanyie tena mipango na tukamwekea kila kitu
sawa.
“Baada ya
kukamilisha, tunashangaa hajaondoka tena, kwa hiyo upande wetu sisi hatujui
kinachoendelea na wala hatuna njia nyingine ya kumsaidia, kama ni suala la
madai basi ni juu ya wakala wake, ndiye anayejua na ndiye anayetakiwa
kufuatilia kila kitu.
“Kapombe
alikuwa na nafasi nzuri kuweza kucheza na kufanikiwa kusonga mbele zaidi kisoka
tofauti na hapa nchini lakini mwenyewe ndiye mwenye maamuzi na kile
kilichotokea na anajua nini kinaendelea,” alisema Wambura.
Akizungumzia
suala la Kapombe, Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage alisema: “Nazionya
klabu nyingine ambazo zinamrubuni kwa kuwa zitajiingiza kwenye matatizo.
“Kapombe
tayari ameshalipwa fedha zake, euro 2,000 alizokuwa akiidai Klabu ya AS Cannes
na Simba itamsafirisha kurejea Ufaransa, kufikia Jumatatu ijayo (Januari 27)
atakuwa ameshaondoka kwenda Ufaransa.”
0 COMMENTS:
Post a Comment