Mashabiki wa soka nchini wamemuona
‘live’ kwa mara ya kwanza Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm na wengi
wakaonyesha kuvutiwa zaidi na kitambi chake.
Awali, mashabiki wengi wa soka
walionyesha kuwa na hamu ya kumuona kocha huyo mwenye umri wa miaka 64 kama
ataweza kumudu mikiki kwenye benchi.
Pluijm akawaonyesha kwamba yuko fiti na
gumzo likahamia kwenye kitambi chake kwamba ‘kinavutia’.
“Aisee kocha yuko fiti, watu wana
wasiwasi wa bure. Ila kitambi chake bwana, sijui kimekaaje,” alisema mmoja wa
mashabiki kwenye kundi la mashabiki wa Yanga waliokuwa Uwanja wa Taifa, juzi.
“Halafu (Ernie) Brandts alikuwa hataki
vitambi, lakini sasa kocha kaja na kitambi, sijui itakuwaje!” alihoji mwingine
na kusababisha wengine wacheke.
Kocha aliyepita wa Yanga, Brandts
alipiga marufuku vitambi katika benchi lake, vitu vingine alivyokuwa anakataa
ni kutumia simu, hasa muda wa mazoezi.
0 COMMENTS:
Post a Comment