Mabingwa wa soka Tanzania, Yanga
wameondoka leo alfajiri kwenda Tanga kuivaa Coastal Union.
Yanga imeondoka na kikosi kizima,
akiwemo Kocha mpya, Hans van der Pluijm ambaye itakuwa ni mechi yake ya kwanza
ugenini baada ya kuingoza Yanga kuifunga Ashanti United bao 2-1.
Meneja wa Yanga, Hafidhi Saleh amesema
wameamua kuondoka alfajiri wakiwa na basi lao ili ikiwezekana wafanye mazoezi leo.
Yanga inaivaa Coastal Union keshokutwa
Jumatano katika mechi inayosubiriwa kwa hamu.
Coastal Union iliyokuwa imeweka kambi
nchini Oman, itakuwa na kazi kubwa ya kujiuliza baada ya kuanza ligi kwa sare
ya bao 1-1 ikiwa hapo Mkwakwani.
Wakati Yanga iliyoanza ligi kwa ushindi
lakini ikacheza vibaya, italazimika kujituma zaidi kwa kuwa mechi ya timu hizo
katika mzunguko wa kwanza ilimalizika kwa sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar.
0 COMMENTS:
Post a Comment