Mauzo
ya tiketi za elektroniki kwa mechi tatu kati ya nne za Ligi Kuu ya Vodacom
(VPL) zitakazochezwa keshokutwa (Januari 27 mwaka huu) tayari yameanza, hivyo
wanatakiwa kununua mapema.
Mechi
hizo ni kati ya Coastal Union na Yanga itakayofanyika Uwanja wa Mkwakwani
jijini Tanga, Kagera Sugar na Mtibwa Sugar itakayochezwa Uwanja wa Kaitaba
mjini Bukoba na ile ya Azam dhidi ya Rhino Rangers kwenye Uwanja wa Azam
Complex.
Kwa
washabiki wa Dar es Salaam watakaokwenda Tanga kushuhudia mechi kati ya Coastal
Union na Yanga wanashauriwa kuanza safari wakiwa na tiketi zao mikononi, hasa
kwa wale watakaonunua kupitia maduka ya Fahari Huduma.
Tiketi
pia zinaweza kununuliwa kupitia mtandao wa M-Pesa kwa kupiga namba *150*03*02#.
Kwa wanaotumia CRDB simbanking wanaingia kawaida kwa *150*03.
Vilevile
tunawakumbusha washabiki kuwa kwa viwanja ambavyo tayari vina mfumo wa tiketi
za elektroniki hakuna tiketi zitakazouzwa uwanjani, hivyo wanaokwenda kwenye
mechi wanatakiwa kuwa na tiketi zao mikononi.
0 COMMENTS:
Post a Comment