Kiungo wa Mbeya City, Kenny Ally, amepewa wiki moja
kuwa nje ya uwanja baada ya kupata majeraha katika kifundo cha mguu (enka)
katika mechi yao dhidi ya Kagera Sugar.
Mbeya
City ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu ya Kagera Sugar
juzi katika mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu mzunguko wa pili uliochezwa katika
Uwanja wa Kaitaba, Kagera.
Akizungumza
na Championi Jumatano, Kocha Mkuu wa
Mbeya City, Juma Mwambusi, alisema kiungo huyo alipata majeraha katika mchezo
huo wa juzi na hivyo atakaa nje wiki moja.
“Kenny
Ally ni kiungo mshambuliaji wa timu yetu aliyeumia katika mchezo wa juzi dhidi
ya Kagera Sugar na atakuwa nje kwa muda wa wiki moja kutokana na majeraha
aliyoyapata.
“Majeruhi
wengine ni kiungo Steven Mazanda ambaye anaendelea vizuri ila sijajua kama
mchezo ujao atakuwepo mpaka nipate ripoti ya daktari. Francis Casto ana tatizo
la kuumia enka pia ila kwa sasa anaendelea vizuri.
“Kwa
upande wa mshambuliaji Mwagane Yeya, anaendelea na matibabu ya nyonga na
hakufanikiwa kucheza mchezo wa juzi lakini maendeleo yake yanaridhisha,” alisema
Mwambusi.
0 COMMENTS:
Post a Comment