OLABA |
Kocha Mkuu wa Ruvu Shooting, Mkenya, Tom Olaba ameponda kiwango
kilichoonyeshwa na timu ya Mbeya City na kudai kuwa wakiendelea kucheza hivyo
hawatafika mbali.
Amesema hayo baada ya mechi ya juzi Jumatano kwenye Uwanja wa
Mabatini, Kibaha baina ya timu hizo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.
Olaba alisema hakupendezewa na namna wapinzani wake walivyokuwa wakicheza
kwa kuwa kila walipokuwa wakigusa mpira, ilikuwa ni faulo, pia wanatumia nguvu
kuliko akili.
“Sikupenda namna walivyokuwa wanacheza, hawana nidhamu uwanjani, yaani
asilimia 65 wanacheza faulo tu na kwa mpira huu hawatafika mbali,” alisema
Olaba.
0 COMMENTS:
Post a Comment